Akida- Itikadi-
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Available in 65 languages
«Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Muadhi akiwa nyuma yake alisema: "Ewe Muadhi bin Jabali", Akasema: Labaika Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema hivyo mara tatu: " Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto", akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je, niwaeleze watu ili wapate habari njema? Akasema: "Ukifanya hivyo, watabweteka". Na alieleza Muadhi jambo hili wakati wa kifo chake kwa kuogopa kupata dhambi za kuficha elimu.»Meaning translation ·
Saved at original quality








