Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
Available in 21 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi" Na katika riwaya ya Muslim: "Hatoacha kuendelea kujibiwa mja madam tu hajaomba dhambi, au kukata ukoo na madam hajafanya haraka" pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka? akasema: "Anasema: Nimeomba, hakika nimeomba, wala sijaona ananijibu, akakata tamaa na wakati huo akaacha kuomba".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwamba hujibiwa mja dua zake madam tu hajaomba kutenda maasi au kukata ukoo, na madam hajafanya haraka, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka kunakoambatana na kuzuiliwa kujibiwa dua?, akasema: ni mtu kusema: Hakika nimeomba, na nimeomba, na nimerudia rudia kuomba, lakini hajanijibu; akafanya haraka wakati huo na akaacha kuomba.

Source
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Download image

Saved at original quality