Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 70 languages
«Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na mtu akiwakopesha watu,basi alikuwa akisema kumwambia kijana wake (Akienda kudai): Ukifika kwa mwenye hali ngumu, basi msamehe, huenda nasi Allah akatusamehe (alipokufa) akakutana na Allah, akamsamehe".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuhusu bwana mmoja aliyekuwa akiamiliana na watu kwa mkopo, au akiwauzia kwa mkopo, Na alikuwa akisema kumwambia kijana wake aliyekuwa akikusanya madeni yaliyoko kwa watu: Utakapomwendea mdaiwa na akawa hana cha kulipa deni analodaiwa kwa sababu ya kushindwa "Basi, msamehe"; Ima kwa kumpa muda zaidi na kutong'ang'ania kumdai, Au kwa kukubali alichonacho hata kama kina mapungufu, na hiyo ni kwa hamu yake na tamaa yake ya kutaka Allah asimuadhibu na amsamehe, Alipofariki Allah akamsamehe na hakumuadhibu kwa makosa yake mengine.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality