Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

Available in 70 languages
«Kutoka kwa Khaula Al-Answariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika watu wanaotumia mali ya Mwenyezi Mungu pasina haki, hao (wana adhabu ya) moto siku ya Kiyama".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu wanaotumia mali ya waislamu kwa batili, na wanaichukua pasina haki, na maana hii inajumuisha kuanzia ukusanyaji wake, na uchumaji wake bila uhalali wake, na utoaji wake katika sehemu zisizo sahihi, na inaingia katika hilo kula mali ya yatima na mali ya wakfu, na kutotunza amana, na kuchukua chochote katika mali ya umma bila ya haki. Ameeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo yao ni moto siku ya Kiyama.

Source
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Download image

Saved at original quality