Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:

Available in 54 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Amekataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- na akatahadharisha kuhusu baadhi ya vitendo vya watu zama za ujinga akasema: Si miongoni mwetu: La kwanza: Atakayepiga mashavu, na ametaja mashavu pekee kwa sababu ndio watu hufanya mara nyingi katika hilo, na vinginevyo kupiga sehemu zingine kunaingia ndani uso. La pili: Kuchana uwazi wa nguo ili aingize kichwa kwa sababu ya huzuni kubwa. La tatu: Akaomboleza kwa maombolezo ya za zama za ujinga kama kujiombea maangamivu na laana, na malalamiko, na makelele na mengineyo.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality