Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abii Waqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

Available in 66 languages
«Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abii Waqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda baadhi ya waja wake, Na miongoni mwao ni mchamungu: Mwenye kutekeleza amri za Allah, mwenye kuyaepuka makatazo yake. Na anampenda mwenye kutosheka: Aliyetosheka kutowahitajia watu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hageuki kwa mwingine. Na anampenda mnyenyekevu: Mwenye kujinyenyekeza, mwenye kumuabudu Mola wake Mlezi, mwenye kujishughulisha na yenye kumnufaisha, ambaye hashughuliki na kutaka yeyote amjue au amzungumze kwa sifa au shukurani.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality