Hadith for the World
Mambo ya Mtume.

Muongozo wa Mtume.

7 hadiths

7 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عائشة رضي الله عنها قالت: كان رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم إذا فَاتَتْهُ الصَّلَاةُ مِنَ الليلِ مِن وَجَعٍ أَوْ غَيْرِهِ، صَلَّى من النَّهَارِ ثِنْتَيْ عَشْرَةَ رَكْعَةً.رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Ya kwamba kuna kundi miongoni mwa wanafunzi wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- waliwauliza wake za Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu amali zake za siri? (walipojibiwa) wakasema baadhi yao: Mimi sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Na mimi sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala juu ya godoro. Hilo likamfikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akamshukuru Mwenyezi Mungu na akamsifia, na akasema: "Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: إِنَّ خَيَّاطًا دَعَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِطَعَامٍ صَنَعَهُ، قَالَ أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ: فَذَهَبْتُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى ذَلِكَ الطَّعَامِ، فَقَرَّبَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خُبْزًا وَمَرَقًا، فِيهِ دُبَّاءٌ وَقَدِيدٌ، فَرَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَتَبَّعُ الدُّبَّاءَ مِنْ حَوَالَيِ القَصْعَةِ، قَالَ: فَلَمْ أَزَلْ أُحِبُّ الدُّبَّاءَ مِنْ يَوْمِئِذٍ.متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Palisemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu waombee dua mbaya washirikina, akasema: "Hakika mimi sikutumwa kuwa mtoa laana, bali nilitumwa kuwa huruma".Imepokelewa Imamu Muslim