Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 47 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa unapoingia mwezi wa Ramadhani hutokea mambo matatu: La kwanza: Hufunguliwa milango ya pepo na haufungwi mlango wowote katika milango hiyo. La pili: Hufungwa milango ya moto na haufunguliwi mlango wowote katika hiyo. La tatu: Hufungwa minyororo mashetani na majini wakaidi, hawaachwi kuendelea na yale waliyokuwa nayo katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani. Na yote hiyo ni kwa kuutukuza mwezi wa Ramadhani, na kumhamasisha mtendaji kukithirisha ibada, kama swala na sadaka, na dhikiri na kusoma Qur'ani na mengineyo; na kujitenga mbali na madhambi na maasi.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality