Hadith for the World
Topic

Fiq'hi na misingi yake.

288 hadiths

288 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن فَضَالَةُ بنُ عُبَيْدٍ وسلمان الفارسي وعقبة بن عامر الجهني رضي الله عنهم مرفوعاً: «كُلُّ مَيِّتٍ يُخْتَمُ على عَمَلِهِ إلا الُمرَابِطَ في سبيل الله، فإنه يَنْمِي لَهُ عَمَلَهُ يوم القيامة، ويُؤَمَّنُ فتنة القبر».رواه أبو داود والترمذي وأحمد من حديث فضالة -رضي الله عنه
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن أبي أوفى رضي الله عنه أَنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم فِي بَعْض أَيَّامه التي لَقِي فيها العدو انتظر، حتى إذا مَالَتِ الشمس قام فِيهم، فقال: «أَيُّها الناس، لا تَتَمَنَّوْا لِقَاء الْعَدُوِّ، وَاسْأَلوا الله الْعافية فَإِذا لَقِيتموهم فَاصْبِرُوا، وَاعلموا أَنَّ الْجَنَّة تحت ظِلال السُّيوف ثُمَّ قَال النَّبِي صلى الله عليه وسلم: اللهمَّ مُنزِلَ الْكتاب، وَمُجْرِيَ السَّحاب، وَهازم الأَحْزاب: اهْزِمهم، وَانصُرنا علَيهم».متفق عليه
عن عَائِشَةُ رضي الله عنها «أَنَّ قُرَيْشا أَهَمَّهُم شَأن المَخْزُومِيَّة التي سَرَقَتْ، فَقَالُوا: مَنْ يُكَلِّمُ فيها رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟، فقالوا: وَمَنْ يَجْتَرِئُ عليه إلا أسامة بن زيد حِبُّ رسول الله صلى الله عليه وسلم فَكَلَّمَهُ أسامة، فَقَالَ: أَتَشْفَعُ فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ الله؟ ثُمَّ قَامَ فَاخْتَطَبَ، فقال: إنَّمَا أَهْلَكَ الذين مِنْ قَبْلِكُمْ أنهم كانوا إذا سرق فيهم الشريف تركوه، وإذا سرق فيهم الضعيف أَقَامُوا عليه الحد، وَأَيْمُ الله: لَوْ أَنَّ فاطمة بنت محمد سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا». وَفِي لَفْظٍ «كانت امرأة تَسْتَعِيرُ المَتَاعَ وَتَجْحَدُهُ، فَأَمَرَ النبي صلى الله عليه وسلم بِقَطْعِ يَدِهَا».متفق عليه
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepigana kwa kutaka kuonekana jasiri, na anayepigana kwa hamasa za ukabila, au anayepigana kwa kutaka kuonekana. Ni yupi kati ya hao anayepigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : «ما من مَكْلُومٍ يُكْلَمُ في سبيل الله، إلا جاء يومَ القيامة، وكَلْمُهُ يَدْمَى: اللَّونُ لَوْنُ الدَّمِ، والرِّيحُ رِيحُ المِسْكِ».متفق عليه
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili", Amesema Salim: Na alikuwa Abuu Huraira akisema: "Au mbwa wa shamba", Naye akawa na shamba.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Thabit bin Dhwahaki- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuunga mkono Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chini ya mti, nakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakaye apa juu ya kiapo cha mila isiyokuwa ya uislamu kwa uongo tena kwa makusudi basi atakuwa kama alivyosema, na atakayeua nafsi kwa kitu chochote ataadhibiwa nacho siku ya kiyama, na hakuna uwajibu juu ya mtu ya kuweka nadhiri katika vile asivyovimiliki" Na katika riwaya nyingine: "Na kumlaani muumini ni sawa na kumuuwa". Na katika riwaya: "Na atakayedai madai ya uongo ili ajichumie (mali) kupitia madai hayo hatomzidishia Mwenyezi Mungu -Mtukufu- isipokuwa upungufu".Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عَبْد اللهِ بن أبي أوفى رضي الله عنهما قال: «غَزَوْنَا مَعَ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم سَبْعَ غَزَوَاتٍ، نَأْكُلُ الْجَرَادَ».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما «أنَّ رسُول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- دَخَل مكَّة مِن كَدَاٍء، مِن الثَنِيَّة العُليَا التِّي بالبَطحَاءِ، وخرج من الثَنِيَّة السُفلَى».متفق عليه
Kutoka kwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
imepokewaKutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"Imepokelewa Imamu Muslim