Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

Available in 61 languages
«Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality