Hadith for the World
Fiq'hi na misingi yake.

Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.

231 hadiths

231 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن فَضَالَةُ بنُ عُبَيْدٍ وسلمان الفارسي وعقبة بن عامر الجهني رضي الله عنهم مرفوعاً: «كُلُّ مَيِّتٍ يُخْتَمُ على عَمَلِهِ إلا الُمرَابِطَ في سبيل الله، فإنه يَنْمِي لَهُ عَمَلَهُ يوم القيامة، ويُؤَمَّنُ فتنة القبر».رواه أبو داود والترمذي وأحمد من حديث فضالة -رضي الله عنه
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن أبي أوفى رضي الله عنه أَنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم فِي بَعْض أَيَّامه التي لَقِي فيها العدو انتظر، حتى إذا مَالَتِ الشمس قام فِيهم، فقال: «أَيُّها الناس، لا تَتَمَنَّوْا لِقَاء الْعَدُوِّ، وَاسْأَلوا الله الْعافية فَإِذا لَقِيتموهم فَاصْبِرُوا، وَاعلموا أَنَّ الْجَنَّة تحت ظِلال السُّيوف ثُمَّ قَال النَّبِي صلى الله عليه وسلم: اللهمَّ مُنزِلَ الْكتاب، وَمُجْرِيَ السَّحاب، وَهازم الأَحْزاب: اهْزِمهم، وَانصُرنا علَيهم».متفق عليه
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepigana kwa kutaka kuonekana jasiri, na anayepigana kwa hamasa za ukabila, au anayepigana kwa kutaka kuonekana. Ni yupi kati ya hao anayepigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : «ما من مَكْلُومٍ يُكْلَمُ في سبيل الله، إلا جاء يومَ القيامة، وكَلْمُهُ يَدْمَى: اللَّونُ لَوْنُ الدَّمِ، والرِّيحُ رِيحُ المِسْكِ».متفق عليه
عن عَبْد اللهِ بن أبي أوفى رضي الله عنهما قال: «غَزَوْنَا مَعَ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم سَبْعَ غَزَوَاتٍ، نَأْكُلُ الْجَرَادَ».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما «أنَّ رسُول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- دَخَل مكَّة مِن كَدَاٍء، مِن الثَنِيَّة العُليَا التِّي بالبَطحَاءِ، وخرج من الثَنِيَّة السُفلَى».متفق عليه
Kutoka kwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abdillahi bin zaidi bin A'swim Al-maaziniy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "paliletwa mashtaka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu anayepata wasiwasi kuwa anapata kitu ndani ya swala (katika vitenguzi vya udhu), Akasema: asiondoke mpaka asikie sauti, au apate harufu".Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake. Na katika lafudhi yao nyingine: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Amani, atakapokaa mmoja wenu katika swala basi na aseme: Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, akisema hivyo, basi dua hii itampata kila mja mwema wa Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu, kisha baada ya hapo atachagua maombi yoyote anayotaka kuomba".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال: خَسَفَت الشمس على زمان رسول الله صلى الله عليه وسلم . فقام فَزِعًا، ويخشى أن تكون الساعة، حتى أتى المسجد، فقام، فصلى بأطول قيام وسجود، ما رأيته يفعله في صلاته قطُّ، ثم قال: إن هذه الآيات التي يُرْسِلُهَا الله عز وجل : لا تكون لموت أحد ولا لحياته، ولكن الله يُرْسِلُهَا يُخَوِّفُ بها عباده، فإذا رأيتم منها شيئا فَافْزَعُوا إلى ذكر الله و دُعَائِهِ وَاسْتِغْفَارِهِ.متفق عليه
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake