Hadith for the World
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.

Twahara - usafi-

18 hadiths

18 hadiths

Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن أمتي يُدْعَون يوم القيامة غُرًّا مُحَجَلِّين من آثار الوُضُوء)). فمن اسْتَطَاع منكم أن يُطِيل غُرَّتَه فَليَفعل. وفي لفظ لمسلم: ((رأَيت أبا هريرة يتوضَّأ، فغسل وجهه ويديه حتى كاد يبلغ المنكبين، ثم غسل رجليه حتى رَفَع إلى السَّاقين، ثم قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: إنَّ أمتي يُدْعَون يوم القيامة غُرًّا مُحَجَّلِين من آثار الوُضُوء)) فمن استطاع منكم أن يطيل غُرَّتَه وتَحْجِيلَه فَليَفعَل. وفي لفظ لمسلم: سمعت خليلي صلى الله عليه وسلم يقول: ((تَبْلُغ الحِليَة من المؤمن حيث يبلغ الوُضُوء)).الرواية الأولى: متفق عليه. الرواية الثانية: رواها مسلم. الرواية الثالثة: رواها مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema: Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Lakitwu bin Swabira -radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
Kutoka kwa mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa kampa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: "Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".Imepokelewa na Abu Daud kwa matamshi haya, na amepokea Bukhari bila ya kuzidisha (baada ya kutwaharika)
عن حذيفة رضي الله عنه مرفوعًا: «فُضِّلْنَا على الناس بِثَلاث: جُعِلَت صُفُوفَنا كصفُوف الملائِكة، وجُعلت لنَا الأرض كُلُّها مسجدا، وجُعلت تُرْبَتُهَا لنا طَهُورا، إذا لم نَجِد الماء. وذَكر خِصْلَة أُخرى».رواه مسلم
عن سمرة رضي الله عنه مرفوعاً: «من توضَّأَ يوم الجُمعة فَبِهَا ونِعْمَتْ، ومن اغْتَسَل فهو أفْضَل».رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه والدارمي وأحمد
عن شريح بن هانئ، قال: أتيتُ عائشة أسألها عن المسح على الخُفَّين، فقالت: عَلَيْكَ بِابْنِ أبِي طالب، فَسَلْهُ فإِنَّه كان يُسَافِرُ مع رسول الله صلى الله عليه وسلم فسألناه فقال: «جَعَلَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيَهُنَّ للمسافر، ويوما وليلة للمُقيم».رواه مسلم
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".Imepokelewa Imamu Muslim
عن سلمان الفارسي قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لا يغتسل رجلٌ يوم الجمعة، ويتطهر ما استطاع من طهر، ويدَّهنُ مِن دهنه، أو يمسُّ من طيب بيته، ثم يخرج فلا يفرِّق بين اثنين، ثم يصلي ما كُتب له، ثم ينصت إذا تكلم الإمام، إلا غُفر له ما بينه وبين الجمعة الأخرى».رواه البخاري