Hadith for the World
Twahara - usafi-

Udhu - kutawadha.

8 hadiths

8 hadiths

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن أمتي يُدْعَون يوم القيامة غُرًّا مُحَجَلِّين من آثار الوُضُوء)). فمن اسْتَطَاع منكم أن يُطِيل غُرَّتَه فَليَفعل. وفي لفظ لمسلم: ((رأَيت أبا هريرة يتوضَّأ، فغسل وجهه ويديه حتى كاد يبلغ المنكبين، ثم غسل رجليه حتى رَفَع إلى السَّاقين، ثم قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: إنَّ أمتي يُدْعَون يوم القيامة غُرًّا مُحَجَّلِين من آثار الوُضُوء)) فمن استطاع منكم أن يطيل غُرَّتَه وتَحْجِيلَه فَليَفعَل. وفي لفظ لمسلم: سمعت خليلي صلى الله عليه وسلم يقول: ((تَبْلُغ الحِليَة من المؤمن حيث يبلغ الوُضُوء)).الرواية الأولى: متفق عليه. الرواية الثانية: رواها مسلم. الرواية الثالثة: رواها مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Lakitwu bin Swabira -radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".Imepokelewa Imamu Muslim