Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:

Available in 60 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo alikuwa akiianza Swala yake kwa baadhi ya dua, miongoni mwa dua hizo zilizoripotiwa ni kauli yake: "Allaahumma baaid bainii wa baina khatwaa yaaya, kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi, Allaahu naqinii min khatwaayaaya, kamaa yunaqqah-thaubal abyadhwa minad-danasi, Allaahuma gh-silnii bil maai wath-thalji wal baradai", Hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amtenge mbali na madhambi ili asije akaangukia ndani yake, hata kusiwe na kukutana nayo, kama vile hakuna kukutana baina ya Mashariki na Magharibi, na ikitokea katumbukia ndani yake, basi amtakase kutokana na madhambi hayo kama uchafu unavyotolewa kwenye nguo nyeupe, na amuoshe dhambi zake na kuupoza miale na joto lake, kwa vitakatishi hivi baridi; Maji, theluji na baridi.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality