Hadith for the World
Swala.

Adh-kaar - yasomwayo- wakati wa swala.

15 hadiths

15 hadiths

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na Ahmad
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عائشة رضي الله عنها أنّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم كانَ يقول في ركوعه وسجودِه: «سبُّوحٌ قُدُّوسٌ رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ».رواه مسلم
Kutoka kwa Ka'b Bin Ujrah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)".Imepokelewa Imamu Muslim
عن علي بن أبي طالب رضي الله عنه أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كان إذا قامَ إلى الصلاة، قال: «وَجَّهتُ وجهي للذي فطر السماوات والأرض حنيفًا، وما أنا من المشركين، إنَّ صلاتي، ونُسُكي، ومَحياي، ومماتي لله رب العالمين، لا شريك له، وبذلك أُمِرتُ وأنا من المسلمين، اللهمَّ أنت المَلِك لا إله إلَّا أنت، أنت ربي، وأنا عبدك، ظلمتُ نفسي، واعترفتُ بذنبي، فاغفر لي ذنوبي جميعًا، إنه لا يغفر الذنوب إلا أنت، واهدني لأحسن الأخلاق لا يهدي لأحسنها إلا أنت، واصرف عني سيئَها لا يصرف عني سيئها إلا أنت، لبَّيْك وسَعْدَيْك، والخيرُ كله في يديك، والشر ليس إليك، أنا بك وإليك، تباركتَ وتعاليتَ، أستغفرك وأتوب إليك»، وإذا ركع، قال: «اللهمَّ لك ركعتُ، وبك آمنتُ، ولك أسلمتُ، خشع لك سمعي، وبصري، ومُخِّي، وعظمي، وعَصَبي»، وإذا رفع، قال: «اللهم ربنا لك الحمد مِلءَ السماوات، ومِلءَ الأرض، ومِلءَ ما بينهما، ومِلءَ ما شئتَ من شيء بعد»، وإذا سجد، قال: «اللهم لك سجدتُ، وبك آمنتُ، ولك أسلمتُ، سجد وجهي للذي خلقه، وصوَّره، وشقَّ سمعَه وبصرَه، تبارك الله أحسنُ الخالقين»، ثم يكون من آخر ما يقول بين التشهُّد والتسليم: «اللهم اغفر لي ما قدَّمتُ وما أخَّرتُ، وما أسررتُ وما أعلنتُ، وما أسرفتُ، وما أنت أعلم به مني، أنت المُقَدِّم وأنت المؤَخِّر، لا إله إلا أنت».رواه مسلم
عن الحكم قال: غَلَب على الكُوفة رجُل -قد سَمَّاه- زَمَنَ ابن الأشْعَث، فأمر أبَا عُبيدة بن عبد الله أن يصلِّي بالناس، فكان يصلِّي، فإذا رَفع رأسه من الرُّكوع قام قَدْر ما أقُول: اللَّهُم ربَّنا لك الحَمد، مِلْءَ السَّماوات ومِلْءَ الأرض، ومِلْءَ ما شِئت من شَيء بعد، أهْل الثَّناء والمَجد، لا مانع لما أعْطَيت، ولا مُعْطِي لما مَنعت، ولا يَنفع ذَا الجَدِّ مِنْك الجَدِّ. قال الحَكم: فَذَكَرت ذلك لعَبد الرَّحمن بن أبي ليلى فقال: سمعت البَرَاء بن عَازب يقول: «كانت صلاة رسول الله صلى الله عليه وسلم وركُوعه، وإذا رفع رأسه من الرُّكوع، وسُجوده، وما بَيْن السَّجدتين، قريبًا من السَّوَاء» قال شُعبة: فذَكَرْتُه لِعَمرو بن مُرَّة فقال: قد رأيت ابن أبي ليلى، فلم تَكن صلاته هكذا.رواه مسلم
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfir lii, warhamnii, wa aafiniii, wahdinii, warzuqniii".Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapoondoka katika swala yake anaomba msamaha mara tatu, na anasema: "Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam", Anasema Walid: Nikasema kumwambia Auzaiy: Ni vipi unaomba msamaha: Akasema: Unasema: Astagh-firullaah, Astagh-firullaah.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa
Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".Imepokelewa Imamu Muslim
عن ابن عمر قال: بينما نحن نصلي مع رسول الله صلى الله عليه وسلم إذ قال رجل من القوم: الله أكبر كبيرًا، والحمد لله كثيرًا، وسبحان الله بكرةً وأصيلًا، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «من القائلُ كلمة كذا وكذا؟» قال رجل من القوم: أنا، يا رسول الله. قال: «عجبتُ لها، فتحت لها أبواب السماء» قال ابن عمر: «فما تركتهن منذ سمعتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول ذلك».رواه مسلم
عن أبي بكر الصديق رضي الله عنه: أنه قال لرسول الله صلى الله عليه وسلم: علمني دعاء أدعو به في صلاتي، قال: "قل: اللهم إني ظلمت نفسي ظلما كثيرا، ولا يغفر الذنوب إلا أنت، فاغفر لي مغفرة من عندك، وارحمني إنك أنت الغفور الرحيم".متفق عليه