Hadith for the World
Swala.

Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiwacha.

5 hadiths

5 hadiths

Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".Imepokelewa na Abu Daud
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa amesema: Iswalini mapema swala ya Lasiri, kwani Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeacha swala ya Lasiri basi yameporomoka matendo yake".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeisahau swala, basi aiswali atakapoikumbuka, haina kafara nyingine isipokuwa hiyo: "Na simamisha swala kwa ajili ya kunitaja mimi" [Twaha: 14].Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".Imepokelewa Imamu Muslim