126 hadiths
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake. Na katika lafudhi yao nyingine: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Amani, atakapokaa mmoja wenu katika swala basi na aseme: Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, akisema hivyo, basi dua hii itampata kila mja mwema wa Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu, kisha baada ya hapo atachagua maombi yoyote anayotaka kuomba".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitufundisha kutaka uchaguzi (kwa Mwenyezi Mungu) katika mambo yetu yote kama anavyotufundisha sura katika Qur'ani, Akisema: "Atakapo dhamiria mmoja wenu kufanya jambo, basi na aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi, kisha aseme: 'Allahumma Inniy As-takhiiruka bi ilmika, wa astaq-diruka biqud-ratika wa as-aluka min fadhw-lika al-adhwiim, fa innaka taqdiru walaa aq-diru wata'alamu walaa a'alamu wa anta allaamul ghuyuub, Allahumma inkunta ta'alamu anna haadhal amru- na atataja jambo lenyewe -Khairun lii fii diiniy wadun-yaaya wamaashii wa aaqibatu amriy (Ajiluhuu wa Aajiluhu) Faq-dirhu lii wayassirhuu lii thumma baarik liiy fiihi, wa in kunta ta'alamu anna haadhal amru sharrun lii fii diiniy wa dun yaaya wa maashiy wa Aaqibatu Amriy Fas-rif-huu anniy was-rifniiy anhu waqdir liyal khaira haithu kaana thummar-dhinii bihi" Tafsiri: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakutaka uchaguzi kupitia elimu yako, na ninakuomba uwezo kupitia uwezo wako, na ninakuomba unipe kutoka katika fadhila zako tukufu, kwani wewe unaweza na mimi siwezi, na unajua na mimi sijui na wewe ni mjuzi wa yaliyofichikana, Ewe Mola wangu ikiwa unajua kuwa jambo hili (Anataja shida yake) ni kheri kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (iwe kwa haraka au kwa kuchelewa) basi nakuomba niwezeshe na unifanyie wepesi kwangu kisha unibariki mimi ndani ya jambo hili, Na ikiwa unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liepushe nami na uniepushe nalo, kisha nipangie heri mahala popote itakapokuwa kisha niridhishe nayo".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini, na hii ni pale mmoja wao atakapo tawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaenda msikitini hakusudii kwa kwenda kwake ila swala, hakuna kinachomnyanyua isipokuwa swala, basi hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa daraja kwa hatua hiyo, na atasamehewa makosa kwa hatua hiyo mpaka atakapoingia msikitini, na anapoingia msikitini huhesabika kuwa yuko ndani ya swala madamu swala ndio bado inayomzuia kutoka, na Malaika humuombea rehema mmoja wenu madamu akiwa bado kakaa mahala aliposwali, wakisema: Ewe Mola wetu muhurumie, Ewe Mola wetu msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu mkubalie msamaha wake, wanaendelea kufanya hivyo kwa muda atakaokuwa hajafanya maudhi yoyote, na madam hajatengua udhu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake