Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

Available in 70 languages
«Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za kusimama usiku wa cheo unaokuwa katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, nakuwa yeyote mwenye kujitahidi ndani yake kwa ibada ya swala na dua na kusoma Qur'ani na kumtaja Allah, akiwa na imani na hayo, na kwa fadhila zilizoelezwa kwayo, akitaraji kwa amali yake malipo ya Allah Mtukufu, si kwa kutaka kuonekana na kusikika, basi husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality