Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

Available in 49 languages
«Kutoka kwa Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikula daku pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama kwenda katika swala, nikasema: Ulipita muda gani baina ya adhana na daku? Akasema: Kiasi cha (kusoma) aya hamsini.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Walikula daku baadhi ya Maswahaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama rehema na amani ziwe juu yake kwenda katika swala ya Alfajiri. Anasi akasema kumuuliza Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake: Kulikuwa na kiwango cha muda gani baina ya adhana na kumaliza kula daku?. Akasema Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake: Kiasi cha kusoma aya hamsini za kati na kati, si ndefu wala fupi, wala si kwa kisomo cha haraka wala cha taratibu.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality