Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema:

Available in 49 languages
«Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na mudi moja: Ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati, wa tende au ngano, kwa kila muislamu; aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na hii ni kwa yule ambaye anachakula kinachozidi kwa siku yake hiyo na usiku wake, kwake yeye na kwa wale anaowahudumia. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala ya Iddi.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality