Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema:

Available in 71 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa swala tano za faradhi za usiku na mchana, na swala ya ijumaa kila wiki, na funga ya Ramadhani kila mwaka, vyote hivi hufuta madhambi madogo madogo yaliyo kati yake, kwa sharti la kuyaepuka madhambi makubwa, Ama madhambi makubwa kama zinaa na kunywa pombe haya hayafutwi isipokuwa kwa toba.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality