Hadith for the World
Mambo yaliyo bora.

Ubora na fadhila za matendo mema.

16 hadiths

16 hadiths

Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hana mja wangu muumini toka kwangu malipo yoyote pindi ninapomchukua kipenzi chake katika familia yake duniani kisha akasubiri (malipo mazuri) zaidi ya pepo".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo".Imepokelewa na Abu Daud
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
عن علي رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقول: « مَا مِنْ مُسْلِم يَعُودُ مُسْلِماً غُدْوة إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِي، وَإنْ عَادَهُ عَشِيَّةً إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبحَ، وَكَانَ لَهُ خَرِيفٌ في الْجَنَّةِ».رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد
عن أنس بن مالك وأبي هريرة رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم فيما يرويه عن ربه عز وجل قال: «إذا تَقَرَّبَ العبدُ إليَّ شِبْرًا تَقَرَّبْتُ إليه ذِرَاعًا، وإذا تَقَرَّبَ إليَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ مِنْهُ بَاعًا، وإذا أتاني يمشي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً».حديث أنس -رضي الله عنه- رواه البخاري . حديث أبي هريرة -رضي الله عنه- متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي ذر رضي الله عنه قال: قيل لرسول الله صلى الله عليه وسلم : أرأيت الرَّجل الذي يعمل العمل من الخَير، ويَحمدُه الناس عليه؟ قال: «تلك عاجِل بُشْرَى المؤمن».رواه مسلم
عن أبي هريرة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَن أصبح منكم اليوم صائمًا؟» قال أبو بكر رضي الله عنه: أنا، قال: «فمن تَبِعَ منكم اليوم جنازةً؟» قال أبو بكر رضي الله عنه: أنا، قال: «فمن أطعم منكم اليوم مسكينًا؟» قال أبو بكر رضي الله عنه: أنا، قال: «فمن عاد منكم اليوم مريضًا؟» قال أبو بكر رضي الله عنه: أنا، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «ما اجتمعن في امرئٍ إلا دخل الجنة».رواه مسلم
عَنْ أَبِي ذَرٍّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَقُولُ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا وَأَزِيدُ، وَمَنْ جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَجَزَاؤُهُ سَيِّئَةٌ مِثْلُهَا أَوْ أَغْفِرُ، وَمَنْ تَقَرَّبَ مِنِّي شِبْرًا تَقَرَّبْتُ مِنْهُ ذِرَاعًا، وَمَنْ تَقَرَّبَ مِنِّي ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ مِنْهُ بَاعًا، وَمَنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً، وَمَنْ لَقِيَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطِيئَةً لَا يُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَقِيتُهُ بِمِثْلِهَا مَغْفِرَةً».رواه مسلم