Hadith for the World
Mambo yaliyo bora.

Ubora wa Elimu.

8 hadiths

8 hadiths

عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كان أخوانِ على عهد النبي صلى الله عليه وسلم وكان أحدُهما يأتي النبي صلى الله عليه وسلم والآخر يَحتَرِف، فَشَكَا الُمحتَرِف أَخَاه للنبي صلى الله عليه وسلم فقال: «لعَلَّك تُرزَقُ بِهِ».رواه الترمذي
Kutoka kwa Anas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake hadithi Marfu'u: "Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea".Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah humpa ufahamu katika dini, mimi ni mgawaji tu, na Allah ndiye anayetoa, na umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «النَّاسُ مَعَادِن كَمَعَادِن الذَّهَب وَالفِضَّة، خِيَارُهُم فِي الجَاهِلِيَّة خِيَارُهُم فِي الإِسْلاَم إِذَا فَقُهُوا، والأَرْوَاحُ جُنُودٌ مُجَنَّدَة، فَمَا تَعَارَفَ مِنْهَا ائتَلَفَ، وَمَا تَنَاكَرَ مِنْهَا اخْتَلَفَ». وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم: «تَجِدُون النَّاسَ مَعَادِن: خِيَارُهُم فِي الجَاهِليَّة خِيَارُهُم فِي الإِسْلاَم إِذَا فَقِهُوا، وَتَجِدُون خِيَار النَّاس فِي هَذَا الشَّأْن أَشَدُّهُم كَرَاهِيَة لَه، وَتَجِدُون شَرَّ النَّاس ذَا الوَجْهَين، الَّذِي يَأْتِي هَؤُلاَء بِوَجه، وَهَؤُلاَء بِوَجْه».الحديث الأول: متفق عليه، ولفظه لمسلم؛ وروى البخاري أوله، وروى آخره عن عائشة -رضي الله عنها-. الحديث الثاني: متفق عليه
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi kwako?" Akasema: Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi. Akasema: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir."Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"Imepokelewa Imamu Muslim