Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokewa kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

Available in 66 languages
«Imepokewa kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah humpa ufahamu katika dini, mimi ni mgawaji tu, na Allah ndiye anayetoa, na umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mwenye kutakiwa kheri na Mwenyezi Mungu basi humruzuku ufahamu katika dini yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mgawaji na msambazaji wa yale aliyopewa na Allah Mtukufu katika riziki na elimu na mengineyo, nakuwa mtoaji halisia ni Allah, na ama asiyekuwa yeye hao ni sababu tu hawawezi kunufaisha ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, nakuwa umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka Kiyama kisimame.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality