Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 53 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amali za maiti hukatika kwa kufa kwake, hayapatikani mema tena baada ya kifo chake isipokuwa kwa mambo haya matatu; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya kupatikana kwake: La kwanza: Sadaka yenye kuendelea thawabu zake na kudumu, isiyokatika, kama wakfu, na kujenga msikiti, na kuchimba visima, na mengineyo. La pili: Elimu wanayonufaika nayo watu, kama kutunga vitabu vya kielimu, au kama kumfundisha mtu, yule naye akaisambaza elimu hiyo baada ya kifo chake. La tatu: Mtoto mwema muumini wa kumuombea dua mzazi wake.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality