Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:

Available in 45 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality