Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

Available in 71 languages
«Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu, Haki ya kwanza katika hizi ni kujibu salamu kwa atakayekutolea salamu. Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa na kumzuru. Haki ya tatu: Kulifuata jeneza kutoka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswalia mpaka makaburini mpaka kuzika. Haki ya nne: Kuitika wito anapomuita kuja katika walima wa harusi na mengineyo. Haki ya tano: Kumuombea dua mwenye kupiga chafya, nako ni kumwambia -Yarhamukallaah- (Akuhurumie Mwenyezi Mungu) atakapomhimidi Allah kwa kusema (Al-hamdulillah): kisha mpiga chafya amjibu: -Yahdiikumullaahu wayuslih baalakum- (Akuongozeni Allah na akutengenezeeni mambo yenu).

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality