Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 62 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yanayomsibu muislamu katika maradhi na msongo na huzuni na misukosuko na majanga na shida mbali mbali na hofu na njaa, hata kama utakuwa ni mwiba utakaomchoma na kumuumiza, hilo kwake linakuwa ni kafara ya madhambi kwake na kifuta makosa.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality