Hadith for the World
Mambo yaliyo bora.

Ubora wa Qur'an tukufu.

5 hadiths

5 hadiths

عن أبي أمامة رضي الله عنه قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ: «اقْرَؤُوا القرْآنَ؛ فَإنَّهُ يَأتِي يَوْمَ القِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِهِ».رواه مسلم
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Umama Al-bahily radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Someni Qur'ani, kwani, itakuja Siku ya Kiyama kama muombezi kwa sahibu wake, Zisomeni Az-Zahraawaini: Al-Baqara na Surat Al-Imran. Kwani, zitakuja Siku ya Kiyama kana kwamba ni mawingu mawili au Ghayayatani (kitu chenye kumpa kivuli mtu kwa juu ya kichwa chake), au kana kwamba ni makundi mawili ya ndege walio katika safu, (sura hizo mbili) zikiwatetea wasomaji wake. Isomeni Surat Al-Baqara. Kwani kuichukua (kuisoma) ni baraka, na kuiacha ni majuto, na wala wachawi hawaiwezi."Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ahmad