Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 59 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Mtume rehema na amani ziwe juu yake, aliwauliza maswahaba zake iwapo wanataka awaongoze katika matendo yatakayowapelekea kupata msamaha wa madhambi, na kufutwa kwake kutoka katika vitabu vya Malaika wenye kuhifadhi, na kupata daraja za juu Peponi? Maswahaba wakasema: Ndio tunataka hivyo. Akasema: Ya kwanza: Kueneza na kukamilisha udhu kwa shida; kama vile baridi, ukosefu wa maji, na maumivu ya mwili, na maji ya moto. Pili: Kupiga hatua nyingi - ambazo ni kati ya miguu miwili- kwenda misikiti iliyo mbali na nyumbani, na kurudi rudi kila wakati. Tatu: Kungoja wakati wa Swala, na moyo kuambatana nayo, na kujitayarisha kwa ajili yake, na kukaa msikitini kwa ajili yake kungojea jamaa, anaposwali hungojea mahali pake pa kuswali kwa ajili ya swala nyingine. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa mambo haya ndiyo Jihadi ya kweli; Kwa sababu yanaziba njia za Shetani juu ya nafsi, na yanatenza nguvu matamanio, na yanaizuia isiingiwe na wasi wasi, hivyo kundi la Mwenyezi Mungu likashinda majeshi ya Shetani kupitia hayo; na hii ndiyo Jihadi kubwa zaidi, kwakuwa imekuwa kama kikosi cha jeshi upande wa maadui.

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality