Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:

Available in 53 languages
«Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Walitukanana na kushutumiana watu wawili mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ukawa mwekundu uso wa mmoja wao na ikavimba mishipa inayozunguka shingo yake. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninajua neno ambalo lau angelisema huyu aliyekasirika basi hasira zingemuondokea, lau angesema: Audhubillaahi mina sh-shaitwanir rajiim - Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani. Akasema: Hivi mimi ni mwendawazimu?! Alidhania kuwa hajilindi na Shetani isipokuwa mwenye wazimu.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality