Hadith for the World
Fiq'hi ya Tabia.

Tabia mbovu.

21 hadiths

21 hadiths

Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «أتدرون من المفلس؟» قالوا: المُفْلِس فينا من لا دِرهَمَ له ولا مَتَاع، فقال: «إن المفلس من أمتي من يأتي يوم القيامة بصلاة وصيام وزكاة، ويأتي وقد شَتَمَ هذا، وقذف هذا، وأكل مال هذا، وسَفَكَ دم هذا، وضرب هذا، فيعطى هذا من حسناته، وهذا من حسناته، فإن فنيت حسناته قبل أن يُقْضَى ما عليه، أخذ من خطاياهم فَطُرِحتْ عليه، ثم طُرِحَ في النار».رواه مسلم
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن ابن عمر رضي الله عنهما مرفوعا: «الظلم ظلمات يوم القيامة». عن جابر رضي الله عنهما مرفوعا: «اتقوا الظلم، فإن الظلم ظلمات يوم القيامة، واتقوا الشُّحَ؛ فإنه أَهْلَكَ من كان قبلكم».حديث ابن عمر -رضي الله عنهما-: متفق عليه. حديث جابر -رضي الله عنه-: رواه مسلم
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno, na wala msitiliane shaka (kwa kuhisiana vibaya), na wala msichunguzane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, na wala msichukiane, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «من الكبائر شَتْمُ الرجل والديه» قيل: وهل يسبّ الرجل والديه؟ قال: «نعم، يسبّ أبا الرجل فيسبّ أباه، ويسبّ أمّه، فيسبّ أمّه».متفق عليه
Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abud-dardaa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama".Imepokelewa Imamu Muslim
Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu. Iliwapelekea kumwaga damu zao, na kuhalalisha yaliyo haramu kwao".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «بينما رجل يمشي في حُلَّةٍ تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ، مُرَجِّلٌ رأسه، يَخْتَالُ في مَشْيَتهِ، إذ خَسَفَ اللهُ به، فهو يَتَجَلْجَلُ في الأرض إلى يوم القيامة".متفق عليه
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ: «لا يدخلُ الجنةَ مَن كان في قلبه مِثقال ذرةٍ من كِبر» فقال رجل: إنّ الرجلَ يحب أن يكون ثوبه حسنا، ونَعله حسنة؟ قال: «إنّ الله جميلٌ يحب الجمالَ، الكِبر: بَطَرُ الحق وغَمْطُ الناس».رواه مسلم
Kutoka kwa Samura bin Jundab na Mughira bin Shu'ba radhi za Allah ziwe juu yao, wamesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo"Imepokelewa na Imamu Muslim katika Utangulizi wake
Kutoka kwa Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba yeye alipita kwa watu miongoni mwa Anbat huko Sham, wakiwa wamesimamishwa juani, akasema: Wamekuwaje? Wakasema: Wamefungwa kwa sababu ya jizia (kodi), akasema Hisham: Ninashuhudia kuwa nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani"Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّ عَلَى صُبْرَةِ طَعَامٍ فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِيهَا، فَنَالَتْ أَصَابِعُهُ بَلَلًا فَقَالَ: «مَا هَذَا يَا صَاحِبَ الطَّعَامِ؟» قَالَ أَصَابَتْهُ السَّمَاءُ يَا رَسُولَ اللهِ، قَالَ: «أَفَلَا جَعَلْتَهُ فَوْقَ الطَّعَامِ كَيْ يَرَاهُ النَّاسُ؟ @مَنْ غَشَّ فَلَيْسَ مِنِّي».رواه مسلم