Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

Available in 63 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wanafiki na uvivu wao wa kuhudhuria swala, hasa hasa swala mbili, Ishaa na Alfajiri, nakuwa laiti wangelijua kiwango cha malipo na thawabu katika kuzihudhuria swala hizo pamoja na jamaa ya waislamu, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa mfano wa kutambaa kwa mtoto kwa mikono na magoti. Bila shaka aliazimia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aamrishe swala ikimiweisimamishwe), na amuweke mtu awasalishe watu badala yake, kisha aondoke akiwa pamoja na watu watakaombebea mizigo ya kuni kwenda kwa watu wasiohudhuria swala ya pamoja (Jamaa) ili awachome wakiwa ndani ya majumba yao; kwa sababu ya ubaya wa waliyoyafanya katika madhambi, -lakini hakufanya hivyo- kwa sababu ndani ya majumba yao kuna wanawake na watoto wasio na hatia, na wengineo miongoni mwa wenye udhuru, wasiokuwa na dhambi.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality