Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:

Available in 62 languages
«Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- neno moja nami nikasema neno jingine, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekufa hali yakuwa anaomba kinyume na Mwenyezi Mungu mungu mwingine, ataingia motoni" Na mimi nikasema: Atakayekufa hali yakuwa haombi mungu mwingine ataingia peponi.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeelekeza chochote katika vile ambavyo vinapasa kuwa vya Mwenyezi Mungu pekee kwa asiyekuwa yeye, kama kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutaka msaada kwa asiyekuwa yeye, na akafa katika hali hiyo basi huyu ni katika watu wa motoni. Na akaongeza bin Masuod radhi za Allah ziwe juu yake kuwa atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika pepo.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality