Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:

Available in 71 languages
«Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Palisemwa ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni mtu gani atakayepata furaha zaidi ya uombezi wako siku ya Kiyama? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilijua kuwa ewe Abuu Huraira hatoniuliza mwingine hadithi hii kabla yako, kwa kile nilichokiona kwako, pupa yako juu ya hadithi, Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mtu mwenye furaha zaidi kuliko wote kwa uombezi wake siku ya Kiyama ni yule atakayesema: "Laa ilaaha illa llaah kwa kutakasa nia toka moyoni mwake" Yaani: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na asalimike na ushirikina na riyaa(kufanya mambo kwa kujionesha).

Source
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Download image

Saved at original quality