Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake:

Available in 39 languages
«Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality