Hadith for the World
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.

Funga.

40 hadiths

40 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo toka kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa na Abii Said Al-khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikula daku pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama kwenda katika swala, nikasema: Ulipita muda gani baina ya adhana na daku? Akasema: Kiasi cha (kusoma) aya hamsini.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu siku kumi za mwisho wa Ramadhani, mpaka alimpomfisha Mwenyezi Mungu, kisha wakakaa itikafu wake zake baada yake.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona msongamano na mtu kazingirwa, akasema: "Nini hicho?", wakasema: Alikuwa kafunga swaumu, akasema: "Si katika wema kufunga safarini", na katika tamko la Muslim: "Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عائشة وأم سلمة رضي الله عنهما «أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يُدْرِكُهُ الفجر وهو جُنٌبٌ من أهله، ثم يغتسل ويصوم ».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «إذا أقبل الليل من هَهُنا، وأَدْبَرَالنهار من ههنا، فقد أفطر الصائم».متفق عليه
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «تُعْرَضُ الأعمالُ يومَ الاثنين والخميس، فَأُحِبُّ أَنْ يُعْرَضَ عَملي وأنا صائم». وفي رواية: «تُفْتَحُ أبوابُ الجَنَّةِ يومَ الاثنين والخميس، فَيُغْفَرُ لكلِّ عبد لا يُشْرِكُ بالله شيئا، إِلا رجلا كان بينه وبين أخيه شَحْنَاءُ، فَيُقَالُ: أَنظِروا هذيْن حتى يَصْطَلِحَا، أنظروا هذين حتى يصطلحا». وفي رواية: «تُعْرَضُ الأَعْمَالُ في كلِّ اثْنَيْنِ وَخَميسٍ، فَيَغْفِرُ اللهُ لِكُلِّ امْرِئٍ لا يُشْرِكُ بالله شيئاً، إِلاَّ امْرَءاً كانت بينه وبين أخِيهِ شَحْنَاءُ، فيقول: اتْرُكُوا هذَيْنِ حتى يَصْطَلِحَا».حديث أبي هريرة الأول رواه الترمذي. والحديثان الآخران هما حديث واحد، رواه مسلم، وكرر لفظة: "أنظروا هذين حتى يصطلحا" ثلاثاً
عن عمرو بن العاص رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «فَصْلُ مَا بَيْنَ صِيَامِنَا وصِيَامِ أهْلِ الكِتَابِ، أكْلَةُ السَّحَرِ».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili, na alikuwa akikutana naye katika kila usiku wa Ramadhani akimsomesha Qur'ani, basi hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na Amani ziwe juu yake- ni mkarimu zaidi kwa mambo ya kheri kuliko hata upepo uliotumwa.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كان رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُفطِر قبْل أن يصلي على رُطَبات، فإن لم تكنْ رُطَباتٌ فَتُمَيْراتٌ، فإن لم تكنْ تُمَيْراتٌ، حَسَا حَسَواتٍ مِن ماء.رواه أبو داود والترمذي وأحمد
عن عائشة رضي الله عنها قالت: لم يكن النبي صلى الله عليه وسلم يصوم مِنْ شهر أكثر من شعبان، فإنّه كان يصوم شعبان كله. وفي رواية: كان يصوم شعبان إلا قليلا.متفق عليه