Hadith for the World
Fiq'hi na misingi yake.

Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.

231 hadiths

231 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن عُمَر رضي الله عنه قال: «اسْتَأْذَنَ الْعَبَّاسُ بن عَبْدِ الْمُطَّلِب رسول الله صلى الله عليه وسلم : أن يبيت بمكة ليالي مِنى، من أجل سِقَايَتِه فأذن له».متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitufundisha kutaka uchaguzi (kwa Mwenyezi Mungu) katika mambo yetu yote kama anavyotufundisha sura katika Qur'ani, Akisema: "Atakapo dhamiria mmoja wenu kufanya jambo, basi na aswali rakaa mbili zisizokuwa za faradhi, kisha aseme: 'Allahumma Inniy As-takhiiruka bi ilmika, wa astaq-diruka biqud-ratika wa as-aluka min fadhw-lika al-adhwiim, fa innaka taqdiru walaa aq-diru wata'alamu walaa a'alamu wa anta allaamul ghuyuub, Allahumma inkunta ta'alamu anna haadhal amru- na atataja jambo lenyewe -Khairun lii fii diiniy wadun-yaaya wamaashii wa aaqibatu amriy (Ajiluhuu wa Aajiluhu) Faq-dirhu lii wayassirhuu lii thumma baarik liiy fiihi, wa in kunta ta'alamu anna haadhal amru sharrun lii fii diiniy wa dun yaaya wa maashiy wa Aaqibatu Amriy Fas-rif-huu anniy was-rifniiy anhu waqdir liyal khaira haithu kaana thummar-dhinii bihi" Tafsiri: "Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakutaka uchaguzi kupitia elimu yako, na ninakuomba uwezo kupitia uwezo wako, na ninakuomba unipe kutoka katika fadhila zako tukufu, kwani wewe unaweza na mimi siwezi, na unajua na mimi sijui na wewe ni mjuzi wa yaliyofichikana, Ewe Mola wangu ikiwa unajua kuwa jambo hili (Anataja shida yake) ni kheri kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (iwe kwa haraka au kwa kuchelewa) basi nakuomba niwezeshe na unifanyie wepesi kwangu kisha unibariki mimi ndani ya jambo hili, Na ikiwa unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na dunia yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, basi liepushe nami na uniepushe nalo, kisha nipangie heri mahala popote itakapokuwa kisha niridhishe nayo".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: مرَّ النَّبي - صلى الله عليه وسلم - بامرَأَة تَبكِي عِند قَبرٍ، فقال: «اتَّقِي الله واصْبِري» فقالت: إليك عَنِّي؛ فَإِنَّك لم تُصَب بِمُصِيبَتِي ولم تَعرِفه، فقِيل لها: إِنَّه النَّبِي - صلى الله عليه وسلم - فأتت باب النبي - صلى الله عليه وسلم - فلم تجد عنده بوَّابِين، فقالت: لم أَعرِفكَ، فقال: «إِنَّما الصَّبرُ عِند الصَّدمَةِ الأُولَى». وفي رواية: «تَبكِي على صبِّي لها».متفق عليه
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".Imepokelewa na Ahmad
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن أمتي يُدْعَون يوم القيامة غُرًّا مُحَجَلِّين من آثار الوُضُوء)). فمن اسْتَطَاع منكم أن يُطِيل غُرَّتَه فَليَفعل. وفي لفظ لمسلم: ((رأَيت أبا هريرة يتوضَّأ، فغسل وجهه ويديه حتى كاد يبلغ المنكبين، ثم غسل رجليه حتى رَفَع إلى السَّاقين، ثم قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: إنَّ أمتي يُدْعَون يوم القيامة غُرًّا مُحَجَّلِين من آثار الوُضُوء)) فمن استطاع منكم أن يطيل غُرَّتَه وتَحْجِيلَه فَليَفعَل. وفي لفظ لمسلم: سمعت خليلي صلى الله عليه وسلم يقول: ((تَبْلُغ الحِليَة من المؤمن حيث يبلغ الوُضُوء)).الرواية الأولى: متفق عليه. الرواية الثانية: رواها مسلم. الرواية الثالثة: رواها مسلم
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala, na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji (Bahili) hasara".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «صلاة الرجل في جماعة تَضعُفُ على صلاته في بيته وفِي سُوقِه خمسا وعشرين ضِعفًا، وذلك: أَنَّه إِذَا تَوَضَّأ، فَأَحسَن الوُضُوء، ثمَّ خرج إلى المسجد لاَ يُخرِجُهُ إلاَّ الصلاة؛ لَم يَخْطُ خُطوَةً إِلاَّ رُفِعَت له بِها درجة، وَحُطَّ عَنهُ بها خطيئة، فإذا صلَّى لم تزل الملائكة تُصَلِّي عليه، ما دام في مُصَلاَّه: اللهُمَّ صَلِّ عليه، اللهم اغفِر له، اللهم ارْحَمه، ولا يزال في صلاة ما انتظر الصلاة».متفق عليه
Kutoka kwa Zaidi bin Khalid radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa na mkazo mkubwa na kudumu na jambo kama alivyokuwa katika rakaa mbili za Alfajiri.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «يَغْفِرُ الله للشَّهيد كُلَّ شيءٍ إلا الدَّين». وفي رواية له: «القَتْل في سَبِيل الله يُكَفِّر كلَّ شيءٍ إلا الدَّين».رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa"Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema: Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.Imepokelewa Imamu Muslim
عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «أيُّكم مالُ وارثِه أحَبُّ إليه من مالَه؟» قالوا: يا رسول الله، ما منَّا أحد إلا مَالُه أحَبُّ إليه. قال: «فإن مالَه ما قدَّم، ومالُ وارثِه ما أخَّر».رواه البخاري