Hadith for the World
Fiq'hi na misingi yake.

Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.

231 hadiths

231 hadiths

Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema: Nilikutana na Thauban muachwa huru wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema: 'Niambie matendo nitakayo yafanya (iwe sababu kwa Allah) kuniingiza Peponi' au alisema, nikasema: matendo mazuri yanayopendeka zaidi kwa Allah, akanyamaza, kisha nikamuuliza akanyamaza, kisha nikamuuliza kwa mara ya tatu akasema: Nilimuuliza hayo Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa" Akasema Maadan: Kisha nikakutana na Abuudardaa nikamuuliza, akanambia mfano wa hayo alionambia Thauban.Imepokelewa Imamu Muslim
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «إذا قَام أحَدُكُم من الليل، فَاسْتَعْجَمَ القرآن على لِسَانه، فلم يَدْرِ ما يقول، فَلْيَضْطَجِع».رواه مسلم
Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.Imepokelewa Imamu Muslim
عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «لا حَسَدَ إلا في اثنتين: رجل آتاه الله مالا، فسَلَّطَه على هَلَكَتِهِ في الحَقِّ، ورجل آتاه الله حِكْمَة، فهو يقضي بها ويُعَلِّمَها». وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لا حسد إلا في اثنتين: رجل آتاه الله القرآن، فهو يقوم به آناء الليل وآناء النهار، ورجل آتاه الله مالا، فهو ينفقه آناء الليل وآناء النهار».حديث ابن مسعود رضي الله عنه: متفق عليه. حديث ابن عمر رضي الله عنه: متفق عليه
عن أبي هريرة ـ رضي الله عنه ـ قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «لا يَلِجُ النارَ رجُل بَكى من خشية الله حتى يَعود اللَّبنُ في الضَّرْع، ولا يَجتمع غُبَارٌ في سبيل الله وَدُخَانُ جهنم».رواه الترمذي والنسائي وأحمد
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja wenu kutokana na kung'atwa na mdudu chungu".Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قيل: يا رسول الله، ما يعدل الجهاد في سبيل الله؟ قال: «لا تستطيعونه» فأعادوا عليه مرتين أو ثلاثًا كل ذلك يقول: «لا تستطيعونه»! ثم قال: «مثل المجاهد في سبيل الله كمثل الصائم القائم القانت بآيات الله لا يَفْتُرُ من صيام، ولا صلاة، حتى يرجع المجاهد في سبيل الله». وفي رواية البخاري: أن رجلاً قال: يا رسول الله، دلني على عمل يعْدِلُ الجهاد؟ قال: «لا أجده» ثم قال: «هل تستطيع إذا خرج المجاهد أن تدخل مسجدك فتقوم ولا تفتر، وتصوم ولا تفطر»؟ فقال: «ومن يستطيع ذلك؟!»متفق عليه، والرواية الثانية للبخاري
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema-: "Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayefunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo toka kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
وعن سالم بن عبد الله بن عمر بن الخطاب رضي الله عنهم عن أبيه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: « نِعْمَ الرَّجُلُ عبد الله، لو كان يُصلِّي من الليل» قال سالم: فكان عبد الله بعد ذلك لا يَنامُ من الليل إلا قليلًا.متفق عليه
Imepokelewa na Abii Said Al-khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikula daku pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama kwenda katika swala, nikasema: Ulipita muda gani baina ya adhana na daku? Akasema: Kiasi cha (kusoma) aya hamsini.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu siku kumi za mwisho wa Ramadhani, mpaka alimpomfisha Mwenyezi Mungu, kisha wakakaa itikafu wake zake baada yake.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona msongamano na mtu kazingirwa, akasema: "Nini hicho?", wakasema: Alikuwa kafunga swaumu, akasema: "Si katika wema kufunga safarini", na katika tamko la Muslim: "Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiitangulizie Ramadhani kwa swaumu ya siku moja wala siku mbili, isipokuwa mtu aliyekuwa akifunga swaumu fulani basi na aifunge".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na mwanaume mwenye uharamu wa kumuoa (ndugu yake)".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عائشة وأم سلمة رضي الله عنهما «أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يُدْرِكُهُ الفجر وهو جُنٌبٌ من أهله، ثم يغتسل ويصوم ».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyezi Mungu kamlisha na kamnywesha".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake