Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 54 languages
«Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala, na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji (Bahili) hasara".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika kila siku inayochomozewa na Jua ndani yake kuna Malaika wawili wanateremka na kunadi, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mwenye kutoa katika njia za utiifu na kwa familia na kwa wageni na sadaka za hiyari mrejeshee na mpe badala bora kuliko kile alichotoa, na umbariki. Na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe bahili mzuiaji uharibifu katika mali yake na uiteketeze mali yake anayoizuia na kutompa mwenye kustahiki.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality