Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:

Available in 60 languages
«Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliporejea kutoka katika Hija ya kuaga, alimwambia mwanamke mmoja wa Ansari ambaye hakuhiji: Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi? Akatoa udhuru kwa sababu walikuwa na ngamia wawili, hivyo mume wake na mwanawe walihiji kwa mmoja wao, na kumwacha mwingine akichota maji kisimani. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akamwambia kuwa kufanya Umra katika mwezi wa Ramadhani ni sawa na malipo ya Hija.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality