Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Akida- Itikadi-

Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:

Available in 51 languages
«Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati amemsikia muadhini baada ya kumaliza adhana: "Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wito huu" nayo ni matamshi ambayo hutumika kuita katika ibada ya Mwenyezi Mungu na swala, "Uliotimia" uliokamilika, wito wa tauhidi na ujumbe, "na swala iliyosimama" yenye kudumu ambayo itasimamishwa hivi punde, "mpe" mgawie, "Muhammadi utetezi" na cheo cha juu peponi ambacho hakimstahiki mwingine ila yeye rehema na amani ziwe juu yake, "na fadhila" cheo cha juu zaidi ya vyeo vya viumbe, "na umfufue" na umpe "nafasi yenye kusifiwa" anayosifiwa mwenye kuwanayo; nao ni utetezi mkuu wa siku ya Kiyama, "uliyomuahidi" kwa kauli yako "Huenda akakufufua Mola wako katika nafasi yenye kusifiwa" ili iwe yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Atakayeomba dua hii atastahiki kuupata utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Kiyama.

Source
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Download image

Saved at original quality