Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Fiq'hi na misingi yake.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

Available in 42 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri" Kisha anasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78].»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba thawabu na malipo ya swala ya mtu katika jamaa pamoja na imamu ni bora kuliko swala ishirini na tano anazoziswali peke yake nyumbani kwake au sokoni kwake, kisha akataja rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa usiku na mchana hukusanyika katika swala ya Alfajiri, kisha anasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake akitoa ushahidi kwa hilo: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78] Yaani: Qur'ani ya Alfajiri huishuhudia Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.

Source
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Download image

Saved at original quality