Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake:

Available in 40 languages
«Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.

Source
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Download image

Saved at original quality