Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:

Available in 70 languages
«Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sababu kubwa zinazowapeleka watu peponi ni mbili: Uchamungu na tabia njema. Uchamungu: Ni mtu kuweka kinga kati yako na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nako ni kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake. Na tabia njema: Inakuwa kwa kukunjua uso na kutenda wema na nakujizuia na kero. Na sababu kubwa zinazowaingiza watu motoni ni mbili nazo ni: Ni ulimi na utupu. ulimi miongoni mwa maasi yake: Ni uongo, kusengenya, kuchonganisha, na mengineyo. Na utupu katika maasi yake: Ni zinaa na kulawiti na mengineyo.

Source
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Download image

Saved at original quality