Hadith for the World
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha

Sifa za pepo na moto.

17 hadiths

17 hadiths

Kutoka kwa Ubada bin -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa Kutoka kwa Ibn Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pepo iko karibu mno kwa mmoja wenu kuliko umbali wa kanyagio la kiatu na kisigino chake, na moto pia hivyo hivyo".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema-: "Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".Imepokelewa Imamu Muslim
عن أنس بن مالك رضي الله عنه مرفوعاً: «يُؤتى بأنعم أهل الدنيا من أهل النار يوم القيامة، فَيُصْبَغُ في النار صَبْغَةً، ثم يقال: يا ابن آدم، هل رأيت خيرًا قطُّ؟ هل مَرَّ بك نَعِيمٌ قطُّ؟ فيقول: لا والله يا رب، وَيُؤْتَى بأشدِّ الناس بُؤسًا في الدنيا من أهل الجَنَّة، فَيُصْبَغُ صَبْغَةً في الجنَّة، فيقال له: يا ابن آدم، هل رأيت بُؤسًا قط؟ هل مَرَّ بك شِدَّةٌ قط؟ فيقول: لا والله، ما مَرَّ بي بُؤْسٌ قطٌّ، ولا رأيت شِدةً قَطُّ».رواه مسلم
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه مرفوعاً: «يُؤْتَى بجهنم يومئذ لها سبعون ألف زِمَامٍ مع كل زمام سبعون ألف ملك يَجُرُّونَهَا».رواه مسلم
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: "Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : « سَيْحَانُ وَجَيْحَانُ وَالفُرَاتُ والنِّيل كلٌّ من أنهار الجنة».رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atanadi mwenye kunadi: "Hakika, mtapata afya nzuri na wala hamtougua milele. Na hakika, mtakuwa hai na wala hamtokufa milele, na hakika mtakuwa vijana na wala hamtazeeka milele. Na hakika, mtastareheka na wala hamtapata shida yoyote milele." Na hayo ndiyo kauli yake Mwenye Nguvu, Mtukufu: "Na wataitwa; (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: "Hakika muumini peponi atakuwa na Hema moja la madini ya lulu lililo wazi urefu wake kwenda juu ni maili sitini, muumini humo atakuwa na wake, akiwazungukia na wala baadhi yao hawawaoni wenzao".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Allah Aliyetakasika na kutukuka: Nimewaandalia waja wangu wema, vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, wala sikio kusikia, wala haijawahi kupita katika fikira ya moyo wa binadamu yeyote" Akasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Basi nafsi yoyote haijui yale waliyofichiwa miongoni mwa mambo yenye kutuliza macho" [As-Sajida: 17).Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن عياض بن حمار المجاشعي رضي الله عنه ، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قال ذات يوم في خطبته: «ألَا إن ربي أمرني أن أُعَلِّمَكم ما جَهِلتم، ممَّا علَّمني يومي هذا، كلُّ مالٍ نَحَلتُه عبدًا حلال، وإني خلقتُ عبادي حُنَفاء كلهم، وإنهم أتتهم الشياطين فاجتالتهم عن دينهم، وحَرَّمت عليهم ما أحللتُ لهم، وأمرتهم أن يُشركوا بي ما لم أُنزِّل به سلطانا، وإن الله نظر إلى أهل الأرض، فمَقَتهم عربهم وعَجَمهم، إلَّا بقايا من أهل الكتاب، وقال: إنما بعثتُك لأبتليَك وأبتلي بك، وأنزلتُ عليك كتابًا لا يغسله الماءُ، تقرؤه نائمًا ويقظان، وإنَّ اللهَ أمرني أن أحرِق قُرَيشًا، فقلت: رب إذا يَثْلُغوا رأسي فيدعوه خُبْزة، قال: استخرجهم كما استخرجوك، واغزهم نُغزك، وأنفق فسننفق عليك، وابعث جيشا نبعث خمسة مثله، وقاتل بمن أطاعك مَن عصاك، قال: وأهل الجنة ثلاثة ذو سلطان مُقْسِط مُتَصَدِّق مُوَفَّق، ورجل رحيم رقيق القلب لكل ذي قربى ومسلم، وعفيف متعفِّف ذو عيال، قال: وأهل النار خمسة: الضعيف الذي لا زَبْر له، الذين هم فيكم تبعا لا يبتغون أهلا ولا مالا، والخائن الذي لا يخفى له طمع، وإن دقَّ إلا خانه، ورجل لا يُصبح ولا يمسي إلا وهو يخادعك عن أهلك ومالك «وذكر» البخل أو الكذب والشِّنظير الفحَّاش».رواه مسلم
عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «عُذِّبت امرأة في هِرَّة سَجَنَتْها حتى ماتت، فدخلت فيها النار، لا هي أطعمتها ولا سَقتها، إذ حبستها، ولا هي تَركتْها تأكل مِن خَشَاشِ الأرض».متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ، وَأَقَامَ الصَّلاَةَ، وَصَامَ رَمَضَانَ كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الجَنَّةَ، جَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوْ جَلَسَ فِي أَرْضِهِ الَّتِي وُلِدَ فِيهَا»، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَفَلاَ نُبَشِّرُ النَّاسَ؟ قَالَ: «إِنَّ فِي الجَنَّةِ مِائَةَ دَرَجَةٍ، أَعَدَّهَا اللَّهُ لِلْمُجَاهِدِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، مَا بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، فَإِذَا سَأَلْتُمُ اللَّهَ فَاسْأَلُوهُ الفِرْدَوْسَ، فَإِنَّهُ أَوْسَطُ الجَنَّةِ وَأَعْلَى الجَنَّةِ -أُرَاهُ- فَوْقَهُ عَرْشُ الرَّحْمَنِ، وَمِنْهُ تَفَجَّرُ أَنْهَارُ الجَنَّةِ».رواه البخاري