Hadith for the World
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha

Kuzitakasa Nafsi.

9 hadiths

9 hadiths

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Kutoka kwa Suhaib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."Imepokelewa Imamu Muslim
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alishika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- bega langu, na akasema: "Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia", Na alikuwa bin Omari akisema: Ukishinda mchana usisubiri asubuhi, na ukiamka asubuhi usisubiri jioni, na chukua fursa ya kuitumia vizuri afya yako kwa ajili ya maradhi yako, na uhai wako kwa ajili ya kifo chako.Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: " Msihusudiane, na wala msipandishiane bei, na wala msichukiane, na wala msitengane, na wala wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu muislamu ni ndugu wa muislamu, asimdhulumu, na wala asimsaliti, na wala asimdharau, ucha Mungu uko hapa" Na huku akiashiria katika kifua chake mara tatu "Yamtosha mtu kuwa ni shari kwake kwa kumdharau ndugu yake muislamu, kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu damu yake, na mali yake, na heshima yake".Imepokelewa Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".Imepokelewa Imamu Muslim
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".Imepokelewa na Muslim na Ahmad
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Kiongozi muadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika misikiti, na watu wawili walipoendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakakutana kwa ajili yake na wakaachana kwa ajili yake, na mwanaume aliyeitwa na mwanamke mwenye wadhifa na uzuri, akasema: Hakika mimi ninamhofu Allah, na mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka usijue kushoto kwake unachotoa kulia kwake, na mtu aliyemkumbuka Mwenyezi Mungu akiwa faragha, yakabubujika machozi macho yake".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake