Hadith for the World
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha

Kuyasema vibaya Maasi.

6 hadiths

6 hadiths

Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokewa kutoka kwa Abdillah Ibn Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo".Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: “Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu ni mfano wa mbeba miski na mfua vyuma. Mbeba miski: atakukaribia utapata harufu nzuri ya marashi yake, au utanunua kwake, na ama mfua vyuma: Ima atachoma nguo zako, au utasikia harufu mbaya.”Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi, na hakika miongoni mwa kutangaza machafu, ni mtu kutenda dhambi usiku, kisha akaamka akiwa kasitiriwa na Mwenyezi Mungu juu ya dhambi hilo, akaanza kusema: We fulani, jana usiku mimi nilifanya kadhaa wa kadhaa, hali yakuwa alilala usiku kucha Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka asubuhi anafunua pazia la Mwenyezi Mungu".Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لعن الله السارق، يسرق البَيْضَةَ فَتُقْطَعُ يده، ويسرِقُ الحَبْلَ فَتُقْطَعُ يَدُهُ».متفق عليه