Fiq'hi na misingi yake.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema:
Available in 51 languages
«Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".»Meaning translation ·
Saved at original quality








