Hadith for the World
Tap the image to view it full size
Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

Available in 54 languages
«Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atanadi mwenye kunadi: "Hakika, mtapata afya nzuri na wala hamtougua milele. Na hakika, mtakuwa hai na wala hamtokufa milele, na hakika mtakuwa vijana na wala hamtazeeka milele. Na hakika, mtastareheka na wala hamtapata shida yoyote milele." Na hayo ndiyo kauli yake Mwenye Nguvu, Mtukufu: "Na wataitwa; (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].»

Meaning translation ·

Explanation

The meaning in a few plain lines

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunadi atanadi kuwaita watu wa peponi wakiwa humo wakineemeka: Hakika leo hii mtapata afya na hamtaugua peponi kamwe, kwa namna yoyote ile yatakavyokuwa madogo maradhi hayo, na hakika mtapewa uhai wala hamtakufa humo milele hata usingizi pia hamtaupata ambao ndio kifo kidogo, na leo mtaishi humo mkiwa vijana na wala hamtozeeka humo milele, nakuwa mtaneemeka humo wala hamtohuzunika milele, na hiyo ni kauli yake Mtukufu: "Na wataitwa (waambiwe) hiyo mbele yenu ndio pepo mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya" [Al-Araf: 43].

Source
Imepokelewa Imamu Muslim
Download image

Saved at original quality